BY ISAYA BURUGU 2ND DEC 2022-Huku mtihani wakitaifa kwa kidato cha nne ukianza rasmo kote nchini hivi leo,Usalama umeimarishwa katika vituo vya mitihani kaunti ya Narok .Kwa mjibu wa kamishana wa kaunti ya Narok Isaac Masinde maafisa wa polisi wakutosha wametumwa kwenye vituo vyote vya mtihani huo kulinda doria wakati zoezi hilo likiendelea.Jumla ya watainiwa  alfu 12444 wanaokalia mtihani huo kote katika kaunti hii ya Narok huku mtihani huo ukifanywa kwenye jumla ya vituo 183.

Wakati huo huo Mtihani wa kitaifa kwa kidato cha nne umeanza kote nchini hivi leo na unatarajiwa kuendelea hadi tarehe 23 mwezi huu.Maafisa mbalimbali wa serikali wanashuhudia shughuli hiyo .Wanafunzi 884,263 wa kidato cha nne kote nchini wanafanya mtihani huo .Kule Kisii wasimamizi wa mtiani huo kwenye vituo mbali mbali vya mtihani kwenye kaunti hiyo wamehimizwa kuwa macho wakati mtihani wenyewe ukiendelea.Kaunti hiyo ina jumla ya vituo 372 vikiwemo viwili kwenye magereza.Jumla ya watainiwa alfu 34,852.Akizungumza wakati wa kuzindua kasha la mtihani huo mjini Kisii mkurugenzi wa elimu Kisii ya kati Cyrus Juma anasema  maafisa wa polisi wako macho kukabiliana na visa vyovyote vya udanganyifu.

December 2, 2022