BY ISAYA BURUGU  10TH JAN 2022-Rais Wiliam Ruto ametoa hakikisho kwa taifa kuwa serikali yake itaendelea kujizatiti kuboreshwa mazingira ya utenda kazi kwa maafisa wa polisi nchini.

Akizungumza  katika   hafla ya kufuzu kwa makurutu wa polisi katika chuo cha utoaji mafunzo kwa maafisa hao wa polisi kilichoko Kiganjo kaunti ya Nyeri, rais pia amewataka maafisa hao kuwa tayari kutekeleza majukumu yao bila upendeleo hofu wala wasiwasi wowote. Usemi wake umetiliwa mkazo na Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki.

.Aidha rais Ruto  amewataka kuheshimu kanuni za katiba kuhusu haki za kibinadamu ili kutekeleza jukumu lao bila kukiuka haki hizo.

Maafisa wanaofuzu leo wamekuwa katika chou hicho kwa muda wa miezi tisa iliyopita ambapo jumla ya maafisa 2881 watafuzu.Kati ya idadi hiyo maafisa 2328 ni wanaume huku waliosalia 543 ni wakike.Itakumbukwa kuwa kwa sasa kunao mtaala mpya wa utoaji mafunzo kwa polisi kuambatana na hali ya leo ulimwenguni mtaala uliyozinduliwa na aliyekuwa Waziri wa usalama wa ndani Fred Matiangi .Bila shaka swala la changamoto mbali mbali zinazowakumba maafisa wa polisi litazungumziwa na wote wataozungumza.

Rais Ruto atakuwa Embakasi kuongoza hafla ya kufuzu kwa maafisa wa polisi wa Utala huku akitarajiwa kurejea Ijumaa kwenye chuo cha mafunzo kwa polisi Embakasi ambapo atongoza kufuzu kwa maafisa wa polisi wa utawala.

 

 

January 10, 2023