BY ISAYA BURUGU 22ND JULY,2023-Idara ya maji katika kaunti ya Tana River kwa ushirikiana na kampuni moja ya kibinafasi inapanga kuweka mitambo ya kusafisha maji katika sehemu ambazo gavana wa kaunti hiyo anataka wenyeji wahamie na pia katika hospitali za eneo hilo.

Kaimu afisa mkuu wa idara yam aji Philip Mumba amesema tayari wamezuru sehemu za nyangwani,mahomo,majengo na weinje kuhamazisha umma kuhusu miradi hiyo ambayo inanuia kutekelezwa kupitia ufadhili wa USAID ili kusaidia wakaazi kupata maji safi.

Mumba amepongeza muradi huo akisema utaisaidia wakaazi kupata maji safi na yaliyotibiwa na kuwaepushia wakaazi hatari ya kupatwa na magonjwa yanayotokana na matumizi ya maji ambayo hayajatibiwa.

July 22, 2023