Vikao vya bunge la kitaifa na lile la Seneti vinatarajiwa kurejelewa tena hio kesho, baada ya likizo ya yapata mwezi mmoja.

Shughuli za siku katika bunge la kitaifa zinatarajiwa kuanza kwa mwendo wa kasi, hasa ikizingatiwa kuwa wabunge wataanza kujadili huhusu mapendekezo yaliyoorodheshwa katika bajeti ya ziada.

Kiongozi wa wengi katika bunge hilo Kimani Ichung’wa alisema kuwa kamati mbalimbali zitalazimika kuharakisha mchakato wake ili kukamilisha zoezi hili kabla ya tarehe moja mwezi kesho.

Katika bunge la seneti, suala la mfumo wa ugavi wa rasilimali baina ya kaunti mbalimbali linatarajiwa kuwasilishwa na kujadiliwa katika vikao vya kesho.

February 13, 2023