Kipindi cha joto kinachoshuhudiwa nchini kinatarajiwa kuendelea kwa muda Zaidi. Idara ya utabiri wa hali ya anga nchini, imesema katika ripoti yake ya utabiri wa siku saba zijazo, ikiweka wazi kuwa kipindi hiki kitaendelea hadi tarehe 20 mwezi huu.

Taarifa hiyo imetoa rai kwa wakenya kuendelea kunywa maji kwa wingi ili kujiweka katika hali sawa ya kiafya, na kujiepusha na matatizo yanayotokana na uhaba wa maji mwilini.

Katika taarifa iliyochapishwa hii leo, viwango vya joto vinatarajiwa kuwa juu ya kiwango cha kawaida kikikadiriwa kuzidi nyuzi joto 30 kwa wastani katika maeneo mengi ya taifa.

February 13, 2023