Vikao vya kuhojiwa kwa makamishna wa IEBC vimeendelea kwa siku ya pili, hii leo ikiwa zamu ya aliyekuwa mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati.

Wakili wa kamishna Irene Masit, Donald Kipkorir, amemuuliza bw. Chebukati iwapo alizungumza na aliyekuwa rais Uhuru Kenyatta kuhusiana na suala la raia wa Venezuela waliokamatwa katika uwanja wa ndege wa jomo Kenyatta wakiwa na vifaa vya uchaguzi.

Aidha Chebukati ameeleza kuwa hakuzungumza naye ila alifanya mkutano mkurugenzi wa DCI pamoja na inspekta jenerali wa polisi.

Chebukati vilevile amefichua kuwa Kamishna Iren Masit alitaka tume hiyo kutilia maanani ombi hilo ambalo pia liliambatana na vitisho kuwa iwapo Wiliam Ruto angetangazwa mshindi basi machafuko yangelitokea. Pia kulikuwa na tangazo kuwa iwapo Chebukati angelifanya jinsi alivyo agizwa angefidiwa vyema.

January 24, 2023