Kiongozi wa taifa Rais William Ruto, ametoa changamoto kwa usimamizi wa chama cha kutetea maslahi ya wafanyikazi nchini COTU, kubadilisha mtazamo wake wa mambo na kuanza kushughulika ili kuhakikisha kuwa wanatengeneza nafasi nyingi zaidi za ajira.

Rais amependekeza njia hii kama mojawapo ya njia bora zaidi za kupunguza idadi ya wakenya wasiokuwa na kazi. Rais aliyasema haya katika kikao na wakuu wa COTU wakiongozwa na mwenyekiti wao Francis Atwoli, kwenye ikulu ya Nairobi kutwa ya leo.

Rais Ruto aliongeza kuwa vyama vya wafanyikazi viungo muhimu vya uundaji wa sera zinazochangia usawa na maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

 

February 14, 2023