UN Security Assembly

Marekani na washirika wake wa magharibi kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, wamesisitiza kwamba katibu mkuu wa umoja huo Antonio Guterres ana haki ya kuchunguza iwapo Urusi ilitumia ndege zisizokuwa na rubani za Iran kuwashambulia raia na mitambo ya umeme nchini Ukraine.

Washirika hao wametupilia mbali madai ya Moscow kwamba mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa atakuwa anakiuka mkataba wa umoja wa Mataifa. Balozi wa Urusi kwenye umoja huo Vassily Nebenzia aliyeitisha mkutano huo wa baraza la usalama alidai kwamba ni baraza hilo tu ndilo lina mamlaka ya kuchunguza akiangazia kifungu cha 100 cha mkataba wa Umoja wa Mataifa kinachosema katibu mkuu hatakiwi kupokea maelekezo kutoka nje ya taasisi hiyo.

Naibu balozi wa Marekani kwenye Umoja huo Robert Wood kwa upande wake amesema hoja ya Urusi haina mashiko huku nayo Ufaransa ikiishutumu Urusi kwa kukiuka mkataba huo kila wakati.

October 27, 2022