By Isaya Burugu,Oct 10,2022-Rais  William Ruto hivi leo jumatatu anatarajiwa kuandaa mazungumzo na mwenzake wa Tanzania Samia Suluhu.Rais Ruto amewasili nchini Tanzania jana kwa ziara  ya siku mbili  baada ya kuhudhuria sherehe ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa taifa la Uganda.

Akiwa nchini Tanzania rais Ruto atakuwa makini  kutafuta mbinu za kupanua fursa za kibiashara na kuongeza ukubwa wa shughuli hizo kati ya Kenya na Tanzania.

Rais Ruto pia anatarajiwa kupigania ajenda ya kuondoa vikwazo vya mpakani kati ya Kmataifa ya kanda ya Afrika mashariki.Akiwa nchini Uganda siku ya jumapili,rais Ruto alihoji kuwa eneo hili lina uwezo mkubwa wa ukuaji iwapo vizuizi vya mipakani katika nchi nchi wanachama vitaondolewa.

Kenya na Tanzania hushirikiana kwenye maswala mbali bali yakiwemo,biashara,usalama,uchukuzi ,na mipango.

Ziara hiyo ya rais Ruto nchini Tanzania itakuwa yatatu kwake barani Afrika baada yake kuzuru,Ethiopia,Uganda na sasa Tanzania.

 

 

October 10, 2022