Wabunge katika Bunge la kitaifa wamejadili hoja ya kufanyia mabadiliko ya kikatiba ili kuwawezesha kurejesha mpango wa maendeleo ya maeneobunge almaarufu CDF.

Katika vikao vya bunge la kitaifa adhuhuri ya leo, wabunge wamesifia mpango wa fedha hizo wakitaka zirejeshwe ili waweze kuwasaidia wananchi katika maeneobunge yao kushuhudia maendeleo. Mpango huu uliharamishwa na mahakama ya upeo kama ulio kinyume cha katiba sasa wabunge wakipania kuuweka sambamba na katiba ya taifa.

November 2, 2022