BY ISAYA BURUGU 2ND NOV 2023- Wafanyikazi wa shirika la posta kaunti ya Nakuru wamefanya mandamano leo kulalamikia kutolipwa mshara kwa muda wa  miezi mitano sasa.

Wakizungumza na wandishi Habari Habari wafanyikazi hao wanasema juhudi za wakuu wao kuingilia  kati kuhakikisha kuwa wanatendewa haki pia hazijafua dafu kwani hakuna hatua iliyochukuliwa.

Wafanyikazi hao wanamlaum mkurugenzi mkuu wa shirika hilo kote nchini John Tonui kwa masaibu yao.Wanasema kuwa hawaamini kuwa hakuna fedha za kuwalipa kwani usimamizi wa shirika hilo umekuwa ukitekeleza maswala mbali mbali ikiwemo kuajiri wafanyikazi wapya huku ukidai kuwa hakuna fedha.

Katika kaunti ya Uasin Gishu hali imekuwa kama hiyo huku wafanyikazi wa shirika la posta wakiandamana mjini Eldoret.Wafanyikazi hao wanashikilia kuwa sharti matakwa yao yatekelezwe kabla warejee kazini.

 

 

 

Share the love
November 2, 2023