BY ISAYA BURUGU,30TH SEPT,2023-Wahudumu wa boda mjini Narok wamesema katu hawatawataendelea kulipa kodi kwa serikali ya kaunti ya Narok iwapo matakwa yao hayatashughulikiwa.

Akizungumza mjini Narok mwenyekiti wa wahudumu wa boda boda Lemayian Punyua amesema serikali ya kaunti ya Narok imekuwa ikiwatoza ushuru lakini hadi sasa hakuna mwavuli ya kuwakinga kutokana na mvua na jua kali .Punyua amesema wamekuwa wakitoa ushuru huku wakihaidi kujenga maeneo ya kujikinga panapo nyesha .

Kauli yake imeungwa mkono na katibu wa kundi hilo Nick Pareyio ambaye amesema wahudumu wa boda boda wamekuwa wakihaidiwa mengi lakini  hakuna linalotekelezwa .

Wahudumu hao aidha wametoa ilani kwa serikali ya kaunti ya hadi mwezi ujao kuhakikisha kuna jambo ambalo limefanyika la sivyo watasitisha mara moja ulipaji ushuru kwa serikali hiyo. Narok Stephen Karmushu ni kiogozi wa boda boda mjini Narok.

 

Share the love
September 30, 2023