BY ISAYA BURUGU,30TH SEPT,2023-Masomo ya maelfu ya Watoto humu nchnin yatadhirika iwapo wizara ya elimu itaendelea mbele na kutekeleza mapendekezo ya jopo la rais kuhusu elimu bila kupitisha sheria hitajika bungeni.

Haya ni kwa mjibu wa mbunge wa Emuhaya Amboko Milemba.Milemba anasema kuwa mengi yalkiyotekelezwa kufikia sasa huenda yakabatilishwa bila sheria hitajika kuundwa.

Milemba amesema kuwa baadhi ya mapendekezo ya jopo hilo  linahitajika kubatilishwa kisheria na hata katiba kupitia kura ya maamuzi iwapo yatatekelezwa.

Jumla lililopita bunge lilisimmaisha utekelezaji wa mapendekzo ya jopo kazi hilo hadi sheria mwafaka ibuniwe.Japo wizara ya elimu kupitia Waziri Ezekiel Machogu ilikuwa imetangazwa kutekelezwa kwa mapendekezo kadhaa.

 

 

 

 

 

Share the love
September 30, 2023