Serikali ya Kaunti ya Narok imetoa onyo kwa wakaazi wanaoishi katika maeneo yanayopakana na mbuga za wanyama pori dhidi ya ugonjwa wa kimeta yaani Anthrax.

Akizungumza afisini mwake waziri wa afya na usafi wa umma katika kaunti ya Narok Antony Lemunkuk alidhibitisha haya kutokana na ripoti rasmi ya vifo vya watu wawili waliokula nyama ya kondoo iliyoathirika na ugonjwa wa kimeta.

Lemunkuk aliyeomboleza na familia za waathiriwa alijuta kuwa kondoo wengine 50 wameonyesha dalili ya ugonjwa huo kijijini humo huku chanjo elfu 20,000 zikitolewa ili kudhibiti ugonjwa huo.

Share the love
September 20, 2023