BY SAIAYA BURUGU 25TH AUG 2023-Washukiwa wawili wa wizi wa kimabavu wanaoaminika kuwa na uhusiano na genge kuu la wahalifu linaloripotiwa kumwibia ajuza wa miaka 76 huko Serem kaunti ya Vihiga  mwezi jana kabla ya kumbaka ajuza huyo na kisha kumuua wamekamatwa.

Patrick Misiko,mwenye umri wa miaka 36, na Christine Jerono, mwenye umri wa miaka 46, walikamatwa na maafisa wa polisi  katika eneo la majengo Vihiga  baada ya kupatikana na simu ya mkononi iliyoibiwa kutoka kwa marehemu wakati wa kisa hicho.

Marehemu alikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Mbale  na majirani  waliosikia mayowe  na furugu  lakini kwa bahati mbaya akafariki  kutokana na majeraha aliyoyapata  alipokuwa akipokea matibabu.Maafisa wa polisi kwa sasa wanawasaka wanachama wa  genge hilo waliosalia ambao hadi hivi sasa wangali mafichoni.

 

 

August 25, 2023