Wakili Paul Gicheru anazikwa hivi leo katika Kijiji cha weda Kabatini eneo bunge la Bahati kaunti ya Nakuru. Gicheru alikuwa anatuhumiwa na mahakama ya ICC kuwahonga mashahidi katika kesi iliyokuwa ikimkumba rais Wiliam Ruto na mwanahabari Joshua Sang .Paul Gicheru alifariki mwezi jana katika hali ya kutatanisha hata ingawa uchunguzi uliyofanyiwa mwili wake haukubainisha moja kwa moja kilichopelekea kifo chake.Tayari mwili wake umewasili kwa mazishi viongozi mbali mbali wakitarajiwa kuhudhuria.

 

 

 

October 6, 2022