Mahakama kuu imetupilia mbali rufaa ya mbunge wa Sirisia John Waluke  sasa hiyo ikiwa na maana kuwa mbunge huyo atahitajika  kutumikia kifungo chake cha miaka 67.

Kifungo hicho alikuwa amepewa na mahakama ya chini.Jaji Esther Maina wa mahakama kuu amesema kuwa upande wa mashtaka umewasilisha Ushahidi wakutosha kudhibitisha kesi  ya ufisadi dhidi ya mbunge huyo na Grace Wakhungu na kwamba rufaa yake haikuwa na uzito wowote.Uamuzi uliyotolewa na jaji Elizabeth Juma mwaka 2020 kwamba wao kama wakurugenzi wa kampuni ya Erras supplies na general contractors kama wangeshindwa kulipa shilingi bilioni mbili wangetumikia kifungo cha miaka 67.

 

 

 

October 6, 2022