BY ISAYA BURUGU,10TH FEB 2023-Serikali ya kaunti ya Narok kwa ushirikiano na serikali ya kitaifa inalenga kuwasajili wakulima wapatao 188,000  wakati wanasubiri kupokea  mbolea ya bei nafuu kutoka kwa serikali.

Kamishna wa kaunti ya Narok Isaac Masinde akiwahutubia wenyeji wa Shangoi eneo la Trasmara magharibi ametoa wito kwa wakulima kufika katika afisi za machifu kwa wingi na kujisajili ili kunufaika na mbolea ya bei nafuu kwa shilingi 3,500 inayotolewa na serikali msimu huu wa upanzi.kamishana huyo  amesema lengo kuu la serikali ni kuhakikisha kuna chakula cha kutosha humu nchini ili  kukabiliana na baa la njaa. 

Wakati huo huo kamishna Masinde ametangaza kuwa rais William Ruto atazindua mbolea ya bei nafuu juma lijalo  lengo kuu la serikali ikiwa ni kuweka mipango kabambe ya  kulinda taifa hili dhidi ya baa la njaa. Hayo yanajiri huku wakulima wakifanya matayarisho kwa msimu wa upanzi kufuatia  kipndi kirefu cha kiangazi kushudiwa katika maeneo mengi  nchini.

 

 

February 10, 2023