BY ISAYA BURUGU,30TH JAN,2023-Serikali ya kitaifa inalenga kujenga nyumba elfu 10 za bei nafuu katika kaunti hii ya narok katika mpango wake wa kuwajengea wananchi nyumba za bei nafuu humu nchini.

Haya ni kwa mujibu wa Rais william Ruto. Akizungumza alipozuru kaunti hii kwa hafla ya maombi ya shukrani iliyoandaliwa na gavana Patrick Ole Ntutu, Ruto alidokeza kwamba zaidi ya vijana elfu 15 wataajiriwa ili kuendesha ujenzi wa nyumba hizo.

Ruto kadhalika alisema mbali na ujenzi huo wa nyumba za bei nafuu vilevile serikali pia inalenga kujenga viwanda katika kila kaunti ili waweze kuongeza dhamani ya mazao yanayokuzwa katika kaunti hizo.

Serikali ya Narok tayari imetenga ardhi ili mradi huo uweze kufanikishwa na wakaazi wa narok kunufaika

 

 

January 30, 2023