Askofu paul Kariuki hii leo amesimikwa rasmi kama askofu wa kwanza wa jimbo jipya la Wote katika uwanja wa shule ya UNOA kule Makueni. Jimbo hili jipya lilimegwa kutoka jimbo la Machakos na likatangazwa kuwa jimbo tarehe 22 mwezi julai mwaka huu.

Akizungumza baada ya kusimikwa kwake Askofou Kariuki amewahimiza waumini kuwa watakifu kwa kila jambo wanalotenda ili kutimiza matakwa ya mwenyezi Mungu.

Kwa upande wake mwakilishi wa papa nchini Kenya na Sudan kusini, askofu mkuu Bert Van Megen ameelezea Imani yake kwa askofu Kariuki akisema kuwa katika miaka iliyopita kazi yake imesifiwa na kuonekana.

Wakati hayo yakijiri makardinali wateule 21 wamesimikwa hii leo na Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis. Makardinali hao wapya wamesimikwa rasmi katika mkutano wa Baraza la Makardinali uliofanyika leo mjini Vatican.

Mnamo tarehe 9 Julai 2023 Papa Francis aliwateua Makardinali wapya 21 kati yao Makardinali watatu wakiwa ni kutoka bara la Afrika ambao ni Askofu mkuu mwandamizi Protase Rugambwa wa Jimbo kuu la Tabora, Tanzania, Askofu mkuu Stephen Ameyu Martin MULLA, Jimbo kuu la Juba, Sudan ya Kusini pamoja na Askofu mkuu Stephen Brislin wa Jimbo kuu la Cape Town, Afrika Kusini.

 

September 30, 2023