Bunge la Kitaifa limealika umma kushiriki katika zoezi la kukusanya maoni kuhusu madai ya udanganyifu kwenye Mtihani wa KCSE wa 2022 ambao matokeo yake yalitolewa mwezi uliopita.

Matokeo yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu mnamo Januari 20 yalizua hisia tofauti kutoka kwa Wakenya, huku wengine wakidai udanganyifu.

Hii ilikuwa baada ya shule katika baadhi ya kaunti kurekodi kile kilichochukuliwa kuwa utendakazi mzuri kupita kawaida. Mfano halisi ulikuwa shule za upili za Nyambaria na Mobamba, zote katika Kaunti ya Nyamira, ambazo zilikuwa na watahiniwa wao wote 488 na 388 mtawalia walipata gredi ya kuingia chuo kikuu.

Kupitia notisi ya umma ya Februari 2, Karani wa Bunge la Kitaifa Samuel Njoroge alisema Kamati ya Elimu imeazimia kufanya uchunguzi wa umma kuhusu madai hayo na kutoa mapendekezo kwa Bunge.

February 2, 2023