BY ISAYA BURUGU 7TH  DEC 2022-Rais  William Ruto amewataka majaji 20 wapaya walioteuliwa kuhudumu katiaka mahakama kuu  kuwatumikia  wananchi  kwa moyo mmoja na kuzingatia maadili ya hali ya juu.Akizungumza katika ikulu ya Nairobi wakati wa kuapishwa kwa majaji hao,Ruto amewataka majaji hao  kuwahudumia wakenya kwa usawa  kama inavyohitajika kikatiba.

Aidha amesema kuwa kufanya kazi kwa afisi ya umma  kunahitaji kujitolea kwa mjibu wa matarajio yaliyo kwenye afisi hiyo.Patricia Nyaundi, Diana Kavedza, Sophie Chirchir na  Mwaisha Said  ni miongoni mwa majaji  waliokula kiapo hicho.

December 7, 2022