BY ISAYA BURUGU,28TH JAN 2023-Watu watatu wamepoteza uhai  kufuatia  ajali mbaya ya barabara baada ya matatu ya uwezo wa kubeba watu 14 ilipogonga lori katika kaunti ya Muranga.

Ajali hiyo imetokea leo asubuhi na kuhusisha  matatu iliyokuwa ikijaribu  kulipita lori  lakini ikaligonga lori hilo.Kwa mjibu wa ripoti .

Matatu hiyo ilikuwa ikisafirisha miraa kwenye barabara ya  Kambiti kwa Muthike.Hata hivyo haikubainika ni watu wangapi waliokuwa kwenye matatu na lori lenyewe

January 28, 2023