Waziri wa Ulinzi nchini Aden Duale, ameanza ziara rasmi ya siku tatu nchini India, katika juhudi za kuimarisha ushirikiano wa kijeshi na kidiplomasia kati ya Kenya na India.
Duale aliwasili nchini India mapema leo, katika izara yake ya kwanza kwenye tifa hilo, na pia ziara ya kwanza ya afisa mkuu wa serikali nchini, tangu Rais William Ruto alipochukua usukani wa Serikali mwaka jana. Taarifa kutoka idara ya ulinzi ya India zinaeleza kuwa waziri Duale amepangiwa kufanya mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa India, Rajnath Singh, hapo kesho. Na hata ingawa haijawekwa bayana yale yatakayaojadiliwa, mazungumzo haya yanadokezwa kuwa huenda yatahusu masuala ya usalama na ushirikiano wa kijeshi kati ya Kenya na India.
Katika kipindi cha ziara yake, Waziri Duale pia atazuru eneo la kuegesha meli la India pamoja na viwanda vya ulinzi katika maeneo ya Goa na Bengaluru.
https://twitter.com/SpokespersonMoD/status/1696019300950442326?s=20