Zoezi la kuwasajili makurutu wa jeshi limeng’oa nanga rasmi hii leo kote nchini huku onyo ikitolewa kwa maafisa wa jeshi na wananchi dhidi ya kujihusisha na masuala ya udanganyifu wakati wa zoezi hilo.

Kwenye kikao na wanahabari, naibu mkuu wa majeshi luteni jenerali Jonah Mwangi alisema idara ya ulinzi iko ngangari kuwakabili wanaojihusisha na ufisadi ili kujiunga na jeshi.

Zoezi hili litaendelea hadi tarehe 8 mwezi ujao. Usajili huo unaendele kwa vituo vipatao 300 katika kaunti 47.

Share the love
August 28, 2023