Naibu rais Rigathi Gachagua kwa mara nyingine amesema kuwa serikali ya rais William Ruto haitazitumia asasi za usalama kuwakandamiza wapinzani wao.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa bwawa la Thiba katika kaunti ya Kirinyaga,Gachagua amesema kuwa hawana mpango wa kuwatumia machifu kuendeleza mambo ya siasa huku akidai kuwa machifu wengi walitumika vibaya wakati wa kampeni za kisiasa.

Itakumbukwa kwamba naibu rais mara kadhaa amekuwa akiikashifu serikali ya rais mstaafu Uhuru Kenyatta kwa kile alichokitaja kama ukandamizaji wa viongozi wa kisiasa waliomuunga mkono rais William Ruto wakati wa uchaguzi wa agosti tisa.

October 15, 2022