Rais William Ruto amemteua Amin Ibrahim Mohammed kama mkurugenzi mpya wa idara ya DCI majuma matatu baada ya George Kinoti kujiuzulu kutoka kwa wadhfa huo.Mohammed alikuwa miongoni mwa watu watatu waliochaguliwa baada ya tume ya huduma kwa polisi NPS kuwahojiwa watu kumi siku ya jumanne.

Kabla ya uteuzi wake,Mohammed alikuwa akihudumu kama mkurugenzi wa idara ya masuala ya ndani katika tume ya NPS.

October 15, 2022