Baraza la maaskofu wa kanisa katoliki KCCB, limewapongeza wakenya kwa kudumisha amani, wakati na baada ya uchaguzi mkuu ulioandaliwa tarehe tisa mwezi agosti mwaka huu. Wakitoa taarifa kwa vyombo vya habari, baraza hilo limewahimiza viongozi waliochaguliwa kuweka kando masuala ya siasa na kuwatumikia wakenya kikamilifu bila ya kuzingatia mirengo waliokuwa wakiegemea.

Kuhusiana na kupanda kwa gharama ya maisha, baraza hilo limeitaka bunge kuangazia suala la ushuru kwa kuhakikisha kuwa wakenya hawatozwi ushuru ya juu hatua ambayo wamesema itapunguza bei ya bidhaa mbalimbali.

Hali kadhalika baraza hilo limejadili suala la ukame ambalo limeathiri mamilioni ya watu humu nchini na kuitaka serikali kuweka mikakati dhabiti ili walioathirika wapate chakula cha msaada huku likiwaomba wakenya wenye nia njema kuendelea kutoa misaada ya aina mbalimbali kwa waathiriwa.

 

November 10, 2022