Abiria waliokuwa na hasira wamewakashfu Waziri Murkomen na mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege nchini Kenya Airways kwa kutoweka mikakati mwafaka ya awali ili kuwaondolea dhiki. Abiria hao waliozungumza katika uwanja wa ndege wa JKIA wamesema usimamizi wa shirika hilo na serikali walikuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa wateja waliokuwa wamepanga safari na hata kulipia nauli zao za ndege kuelekea katika sehemu mbali mbali za ulimwengu hawatatiziki na mgomo huo.

Kupitia mtandao wa twitter, Shirika hilo lilisema kuwa limelazimika kuwahudumia abiria ambao wanapaswa kusafiri nadni ya saa 48 huku wakiomba msamaha kwa abiria ambao wamegahdhabishwa na matukio hayo ya leo.

 

November 5, 2022