Aliyekuwa bingwa wa mbio za Marathon Kelvin Kiptum amezikwa hii leo katika eneo la Naiberi kaunti ya Uasin Gishu. Hafla ya mazishi ya mwanariadha huyo ilihudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serikalini akiwamo rais William Ruto na naibu wake Rigathi Gachagua miongoni mwa wengine.

Rais Ruto akitoa rambirambi zake, amemsifia Kiptum kama mtu mchapa kazi na aliyejitolea kuhakikisha kuwa Kenya inatambulika kwenye mbio za marathon kwa kuvunja rekodi ya dunia.

Hali kadhalika Ruto amewashauri wanariadha waliohudhuria mazishi hayo kujiepusha na matumizi ya dawa za kusisimua misuli.

Kwa upande wake Naibu rais Gachagua ameshikilia kujitolea kwa serikali katika kuimarisha maslahi ya wanariadha humu nchini.

February 23, 2024