Vikao vya UNEA 6

Awamu ya sita ya kongamano la Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA), imeng’oa nanga asubuhi ya leo katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) eneo la gigiri katika kaunti ya Nairobi.

Kongamano hilo la siku tano litawaleta pamoja wajumbe wapatao 5,000 kutoka mataifa 193 wanachama, ili kujadili kuhusu ushirikiano wa pande mbalimbali katika kukabiliana na suala la mabadiliko ya hali ya hewa, uchafuzi wa mazingira sawa na suala la taka.

Waziri wa mazingira humu nchini Soipan Tuya ni miongoni mwa wawakilishi wa Kenya akitarajiwa kuwa mmoja wa watakaoongoza majadiliano kwenye kongamano hilo. Rais wa UNEA-6 na ambaye pia waziri wa nishati wa Morocco, Leila Benali katika hotuba yake ya ufunguzi amesema utunzaji wa mazingira ni jukumu la pamoja.

SOMA PIA: Naibu rais apendekeza mfumo wa hukumu ya kuhifadhi mazingira kwa wakosaji wadogo.

Awamu hii ya sita ya UNEA inafuatia kongamano la awamu ya tano lililofanyika jijini Nairobi kuanzia Februari 28 hadi Machi 2, 2022. Kongamano hilo llilifikia kilele chake kwa kupitishwa kwa maazimio 14, na kuweka mipango ya kuafikiwa kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ifikapo 2030.

Fuatilia Matukio kwenye Kongamano hilo : BOFYA HAPA

February 26, 2024