Naibu Rais Rigathi Gachagua amesema serikali inapania kuwabadilisha maafisa wa Huduma ya Kitaifa ya Polisi wanaolinda vituo muhimu na maafisa wa Huduma ya Kitaifa ya Vijana.

Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho ya Huawei katika jumba la Kimataifa la Mikutano KICC, Gachagua amesema maafisa wa polisi wanahitaji kutumwa kote nchini ili kupambana na ujambazi na uhalifu.

Gachagua ameongeza kuwa maafisa wa NYS wana nidhamu ya kutosha kushughulikia majengo ambayo kwa muda mrefu yamekuwa chini ya uangalizi wa Polisi.

Naibu rais aliandamana na viongozi mbalimbali akiwemo waziri wa michezo Ababu Namwamba.

December 15, 2022