Wazee wa jamii ya Maa kutoka eneo la Ewaso Kedong, Kaunti Ndogo ya Kajiado Magharibi, wameelezea wasiwasi wao kuhusu kuongezeka kwa visa vya uchinjaji haramu wa punda katika eneo hilo. wakizungumza kwenye kikao kilichoandaliwa na shirika la Farming Systems Kenya kwa ufadhili…
Maafisa wa polisi wameeleza utayari wao wa kuhakikisha usalama na pia kukabiliana na maandamano yaliyoratibiwa kuandaliwa siku ya Alhamisi. Maandamano hayo yamepewa jina la Nane Nane. Kaimu Inspekta Jenerali wa Polisi nchini Gilbert Masengeli, alisema haya baada ya kuongoza kikao cha maafisa…
Douglas Kanja ambaye amekuwa akihudumu kama kaimu Inspekta jenerali wa polisi kwa majuma mawili, sasa ameteuliwa rasmi kutwaa wadhfa huo ambao uliachwa wazi kufuatia kujiuzulu kwa Japhet Koome baada ya shinikizo kutoka kwa wakenya. Kupitia taarifa, mkuu wa utumishi wa umma Felix…
Tume ya Kitaifa ya Huduma ya Polisi (NPSC) imechapisha majina nane ya maafisa walio na nia ya kutwaa nyadhifa za Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi wa Kitaifa (NPS) na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi ya Utawala (APS). Nafasi hizo ziliachwa wazi wiki…
Idara ya Polisi nchini imetangaza kupiga marufuku shughuli za maandamano katikati mwa jiji la Nairobi. Kaimu Inspekta Generali wa Polisi, Douglas Kanja, alitoa tangazo hilo kupitia taarifa rasmi siku ya Jumatano. Kanja alieleza kuwa maafisa wa polisi wamekuwa na wakati mgumu katika…
Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 24 katika Kaunti ya Narok, amehukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kumnajisi mvulana wa miaka 15. Mary Yamati Njoki alifikishwa mbele ya Hakimu Mkuu wa Narok, Phillis Shinyada, ambapo alihukumiwa…
Rais William Ruto amelivunja baraza lake la mawaziri katika mabadiliko ya hivi punde aliyotangaza muda mfupi uliopita. Katika tangazo hilo ambalo halikutarajiwa, kiongozi wa taifa ametangaza kuwatimua mara moja mawaziri wote isipokuwa waziri wa mahusiano ya kigeni Musalia Mudavadi. Uamuzi huu ulionekana…
Rais William Ruto ametia saini mswada wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuwa sheria katika hafla iliyoandaliwa kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa KICC asubuhi ya leo. Mswada huo, ambao ulipitishwa na mabunge yote mawili, unatoa mwongozo wa jinsi…