Rais William Ruto atangaza masharti mapya yatakayosaidi kupunguza matumizi serikalini.

Ofisi za wachumba wa rais, naibu wa rais na mkuu wa mawaziri hazitaendelea kupokea mgao wa fedha kutoka kwa bajeti ya kitaifa. Haya yametangazwa na rais William Ruto. Akilihutubia taifa katika ikulu ya Nairobi, rais Ruto ameeleza kuwa hatua hii inanuia kupunguza…

Mahakama Kuu Yairuhusu Jeshi la KDF Kushirikiana na Polisi Kudumisha Amani.

Jeshi la Taifa litaendelea kusaidiana na maafisa wa polisi katika shughuli za kudumisha amani humu nchini. Hii ni baada ya Mahakama Kuu hapo jana kutoa uamuzi unaoruhusu jeshi kuendeleza shughuli hizo, na kufuta kesi iliyokuwa imewasilishwa na Chama cha Mawakili Nchini (LSK).…

Ushuru wa asilimia 16 kwenye bidhaa za mkate waondolewa.

Mwenyekiti wa kamati ya fedha katika bunge la kitaifa Kimani Kuria amewasilisha bungeni ripoti ya maoni ya wakenya kuhusu mswada wa fedha wa mwaka 2024. Wabunge watapata fursa ya kujadili ripoti hiyo kabla ya kupiga kura ya kuuidhinisha au kuuangusha siku ya…

Jaji mkuu Martha Koome asema shuguli za mahakama hazitasitishwa.

Jaji mkuu Martha Koome amesema kuwa shuguli za mahakama hazitasitishwa kuanzia tarehe 19-21 mwezi huu kama ilivyotangazwa jana na baadhi ya maafisa wa idara ya mahakama. Kupitia taarifa, Koome ameeleza kuwa mahakama ya makadara tu ndio itasalia kufungwa kufutia ujenzi ambao unaendelea…

Rais Ruto arejea

Rais Ruto Arejea Nchini Baada ya Ziara ya Italia na Switzerland

Kiongozi wa taifa Rais William Ruto amerejea nchini asubuhi ya leo baada ya kukamilisha ziara rasmi katika mataifa ya Italia na Switzerland. Katika ziara hizo, Rais Ruto alihudhuria Mkutano wa Kundi la Nchi Saba Tajiri Duniani (G7) pamoja na Kongamano la Kimataifa…

Rais William Ruto na Naibu Rais Rigathi Gachagua wapata alama ya D katika utendakazi wao.

Rais William Ruto na Naibu Rais Rigathi Gachagua wamepata alama ya D katika utendakazi wao. Hii ni kulingana na kura ya maoni ya iliyotolewa na kampuni ya utafiti ya InfoTrak. Utafiti huo uliotolewa leo pia imeonyesha kuwa waziri wa usalama wa ndani…

Wanahabari awapongeza waandishi wa habari kwa kutangaza taarifa za Amani.

Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki amewapongeza waandishi wa habari kwa kutangaza taarifa za Amani na kudumishwa kwa usalama kote nchini. Akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua awamu ya nne ya ruwaza ya mwaka 2030 katika kaunti ya Marsabit, Kindiki ameeleza…

Serikali yapunguza bajeti ya jumla ya mwaka huu wa kifedha kwa KSh132.46 bilioni.

Serikali imepunguza bajeti ya jumla ya mwaka huu wa kifedha kwa KSh132.46 bilioni kutoka KSh3.981 trilioni hadi KSh3.848 trilioni. Hili ni punguzo la asilimia 3.3. Tangazo hili lilitolewa wakati Rais William Ruto alipotia saini kuwa sheria Mswada wa bajeti ya ziada wa…