Rigathi Gachagua

Naibu wa rais Rigathi Gachagua, ameahidi kwamba serikali itashirikiana kwa ukaribu na wizara ya elimu Pamoja na baraza la kitaifa la mitihani KNEC kuhakikisha kwamba mitihani ya kitaifa itaendelea kwa njia isiyokua na changamoto zozote.

Akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa kipindi cha mitihani ya kitaifa katika jingo la Mtihani Jinini Nairobi, Gachagua amewapongeza washikadau kwa kujitolea kwa hali na mali katika kuhakikisha kuwa wanafunzi wanafanikiwa kuifanya mitihani yao kwa njia inayofaa.

Naibu wa Rais aliandamana na viongozi wengine wanaojumuisha Waziri wa Elimu Eliud Machogu, Mwenyekiti wa Baraza la KNEC Prof. Dkt Julius Nyabudi, na Mkurugenzi Mtendaji wa KNEC Dkt. Njengere.


Mitihani ya kitaifa inatarajiwa kung’oa nanga tarehe 21 mwezi huu hadi tarehe 23 Disemba kwa KCSE huku mitihani ya KCPE ikitarajiwa kuanza tarehe 25 hadi 30 mwezi huu.

November 11, 2022