Gavana wa kaunti ya Narok Patrick Ole Ntutu amesema kuwa serikali yake inapania kukarabati barabara Zaidi katika maeneobunge ya Narok ili kurahisisha usafiri.Akizungumza wakti wa hafla ya maadhimisho ya mashujaa katika shule ya msingi ya DEB eneo la Kilgoris, Ntutu amesema kuwa tayari wamebuni kamati maalum itakayosimamia mradi huo. Kando na hayo Ntutu amewahakikishia wakulima kuwa mbolea za bei nafuu zilizotolewa na serikali tayari zimewasili katika kaunti ya Narok.

Naye seneta wa kaunti hii Ledama Ole kina aliyehudhuria hafla hiyo, amemuomba gavana Ntutu kuhakikisha kuwa mpango wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu unaidhinishwa humu Narok ili kuwasaidia wakaazi wasiojiweza.

Mwingine aliyehudhuria hafla hiyo ni kaunti kamishna wa Narok Bw. Isaac Masinde ambaye ameshikilia kwamba hakuna yeyote atakayeruhusiwa kurejea katika msitu wa mau kama ilivyoagizwa na mahakama ya Narok. Kuhusiana na suala la kiangazi inayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi, Bw.Masinde ameeleza kuwa wameweka mikakati dhabiti kuhakikisha hakuna mkaazi wa Narok anayepoteza maisha kutokana na njaa.Aidha amedokeza kuwa kufikia sasa takriban familia 115,000 zinakabiliwa na njaa.

 

October 20, 2022