Kupitia kwa wahudumu wa afya wa kujitolea waliopewa mafunzo maalum, maisha ya wanajamii hawa yameshuhudia mabadiliko ya kipekee huku sasa wakijiepusha zaidi na tabia ya ulaji wa nyama ya mifugo waliofariki. Pia wamekumbatia ujenzi na matumizi ya vyoo, jambo ambalo limewasaidia katika kuepuka magonjwa kama vile kipindupindu. Bw. Jeremiah Sindi ni mmoja wa wahudumu wa afya wa kujitolea katika jamii hii ambaye amekua akiwaelimisha wanakijiji jinsi ya kuishi maisha yasiyo na magonjwa, kwa kukumbatia maagizo na mwongozo wa maafisa wa afya.