Rais William Ruto ameongoza maadhimisho ya 59 ya siku ya mashujaa katika bustani la Uhuru jijini Nairobi hii leo.Hii ni sherehe ya kwanza ya kitaifa kuongozwa na rais Ruto tangu alipoapishwa kama rais wa tano wa taifa hili.Ruto ameahidi kufanya kazi na viongozi wote waliochaguliwa kwenye uchaguzi wa agosti tisa ili kufanikisha maendeleo ya Kenya.

Kuhusiana na suala la ufisadi,Ruto amesema kuwa serikali yake inakusudia kudhihirisha dhamira yake ya kutovumilia ufisadi kwa kuwawajibisha watumishi wote wa umma .Zaidi ya watu 20,000 walihudhuria hafla hiyo.Siku hii huadhimishwa kila mwaka ili kuwakumbuka na kuwasherehekea wakenya waliopigania uhuru wa Kenya.

October 20, 2022