Rais William Ruto ameweka wazi kuwa anapania kuimarisha maswala ya kidigitali na kiteknolojia humu nchini, ili kufungua nafasi zaidi za ajira ili kuinua Maisha ya wakenya wanaopata kipato chao kupitia njia za kidijitali.

Akizungumza katika chuo cha mafunzo ya anuwai cha Kabete, Rais Ruto amesema kuwa serikali imeanzisha mpango wa kuhakikisha kuwa huduma zake zote muhimu zinapatikana mtandaoni katika kipindi cha miezi sita ijayo, kama mojawapo ya njia za kukuza uchumi wa kidijitali.

Zaidi ya hayo, rais amefichua kua atatumia maadhimisho yam waka huu ya sikukuu za Jamhuri kuwaalika magwiji wa kidijitali kutoka kote ulimwenguni ili kusaidia kupiga jeki ulingo huu.

December 6, 2022