Idadi ya wakenya wanaotumia bhangi imeongezeka kwa asilimia 90 ndani ya miaka mitano iliyopita. Haya ni kwa mujibu wa utafiti wa hivi punde uliofanywa na mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya nchini NACADA.

Utafiti huo wa kitaifa kuhusu matumizi ya dawa za kulevya nchini wa mwaka 2022 pia umebaini kuwa mkenya mmoja kati ya wakenya 53 wenye umri kati ya miaka 15-65 hivi sasa wanatumia dawa za kulevya.

Maeneo ambayo yamerekodi idadi ya juu ya watu wanaotumia dawa hizi ni pamoja na Nairobi ambayo inaongoza kwa asilimia 6.3 ikifuatiwa na maeneo ya Nyanza na pwani ambayo yamerekodi asilimia 2.4 na 1.9 mtawalia.

Kuhusu uraibu wa pombe, utafiti huo umeonyesha kuwa watu milioni 1.3 nchini wana uraibu wa pombe huku watoto wenye umri wa miaka 7-9 wakianza kutumia pombe. Hali kadhalika eneo la magharibi linaongoza kwa uraibu wa pombe haramu.

September 11, 2023