Radio Osotua › Local News

Ijumaa yatangazwa kama siku ya likizo ya umma kwa maadhimisho ya Idd-ul-Fitr.

Local News April 19, 2023 John Waicua

Waziri wa usalama wa Ndani Kithure Kindiki ametangaza kuwa siku ya Ijumaa, Aprili 21 itakuwa sikukuu ya umma ili kutoa nafasi kwa waumini wa dini ya kiksristu kusherehekea Idd-ul-Fitr.

Tangazo hilo limechapishwa katika notisi ya gazeti la serikali iliyochapishwa hii leo kwa mujibu wa kifungu cha 2 (1) cha Sheria ya Likizo ya Umma. Sikukuu ya Eid al-Fitr, ni sikukuu muhimu kwa waumini wa dini ya kiislamu ulimwenguni kote ambayo inaadhimisha mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.