Serikali imetakiwa kuweka mikakati itakayohakikisha kuwa wakenya wanalindwa kutokana na bei ya juu ya mafuta katika siku zijazo. Wakitoa taarifa kuhusu hali ya taifa, maaskofu wa kanisa katoliki wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza la maaskofu KCCB, askofu mkuu Maurice Muhatia, wamesema kuwa ongezeko la mafuta, linaathiri pakubwa sekta zote nchini hasa zile muhimu, hatua ambayo wanasema itachangia kuyumba kwa Uchumi wa taifa.
Hali Kadhalika, maaskofu wametoa wito kwa wizara ya afya kushugulikia madeni yanayodaiwa na hospitali za kidini chini ya bima ya zamani ya NHIF, wakieleza kuwa wanadai serikali zaidi ya shilingi bilioni 5.7, hali wanayosema imeathiri pakubwa utoaji wa huduma za matibabu katika hospitali za kidini.
Kuhusu suala la usajili wa wapiga kura, KCCB imewahimiza wakenya na hasa vijana kujisajili kama wapiga kura ili waweze kushiriki uchaguzi mkuu ujao kwa kuwachagua viongozi wanaowataka.
| KCCB Press statement | 14th April 2026
“We particularly appeal to our young people to make all efforts to get a voters card….This is one way of voicing your concerns by the choices you will make for a better Kenya. Take your civic mandate seriously and register in readiness… pic.twitter.com/nJYbRFMNld— KCCB – Catholic Justice & Peace Department (@CJPDKENYA) April 16, 2026
— KCCB – Catholic Justice & Peace Department (@CJPDKENYA) April 16, 2026

