Radio Osotua › Local News

IEBC Yaibua Wasiwasi Kuhusu Hali Ya Kisiasa Nchini.

Local News April 15, 2026 Brigit Agwenge

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imeibua wasiwasi kuhusu hali ya kisiasa ya sasa nchini, ikionya kwamba masuala kama vile uhuni na  kutoaminiana yanaweza kudhoofisha uendeshaji wa uchaguzi ujao.

Wakizungumza wakati wa mkutano wa kifungua kinywa kati ya Muungano wa Sekta ya kibinafsi KEPSA na IEBC siku ya Jumatano, wadau waliashiria kuongezeka kwa hofu kuhusu vurugu za kisiasa sawa na kuongezeka kwa ushawishi wa pesa katika uchaguzi.

Vilevile waliashiria kile walichokielezea kama utamaduni wa uhuni ambapo wanasiasa wanadaiwa kuwatumia vijana kusababisha ghasia.