Japheth Koome

Kamati ya Pamoja ya uteuzi kutoka bunge la seneti na bunge la kitaifa, imeidhinisha uteuzi wa Japheth Koome kama inspekta jenerali wa polisi, baada ya kukamilisha shughuli ya kumpiga msasa hio jana.

Koome ambaye alikua kamanda wa polisi katika chuo cha mafunzo ya polisi cha Kiganjo, aliteuliwa kutwaa wadhifa huo baada ya mtangulizi wake Hillary Mutyambai kuchukua likizo ya muda mrefu kutokana na matatizo ya kiafya.

Baada ya kuidhinishwa, sasa koome anasubiri uteuzi rasmi kutoka kwa rais William Ruto kabla ya kuanza kutekeleza jukumu lake, huku akitarajiwa kuanza wajibu wake kwa kutegua kitendawili cha mashambulizi ya mara kwa mara hasa katika maeneo ya kaskazini mwa taifa.

SAUTI: Maseneta waijadili hoja ya Kumuidhinisha Japheth Koome

November 9, 2022