Radio Osotua › Local News

Jinamizi la ajali:Wanafunzi 6 waaga dunia kwenye ajali Naivasha

Local News April 18, 2023 Osotua

BY ISAYA BURUGU,18TH APRIL,2023-Takriban wanafunzi 6 wamefariki kufuatia ajali mbaya ya barabarani eneo la Delamare Naivasha kaunti ya Nakuru.

Wanafunzi hao walikuwa wakisafiri kutoka Magharibi mwa Kenya kuelekea Nairobi ajali ilipotokea.

Sita hao walikufa papo hapo.

Ajali hiyo ilihusisha lori na matatu iliyokuwa imewabeba wanafunzi hao.

Wengine 10 waliojeruhiwa wamekimbizwa katika hospitali ya kaunti ya Naivasha kwa matibabu.