Waziri wa habari, mwasiliano na uchumi wa kidijitali Eliud Owalo ameeleza kuwa Serikali imewezesha mchakato ambapo kampuni za mawasiliano zitakusanyika pamoja, licha ya kuwa washindani sokoni, na kuanza mpango kabambe wa kutengeneza simu za kisasa za bei nafuu katika soko la Kenya.

Akizungumza alipokuwa akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo ya mwaka wa fedha 2023/2024, Owalo amesema watahakikisha kwamba usalama wa mtandao hautatizwi ili data inayotoka kwa umma iwe salama na kulindwa huku serikali ikipania kuweka huduma zote za serikali kwa mfumo wa kidigitali.

February 13, 2023