Kenya imeungana na ulimwengu kuadhimisha siku ya redio,kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa redio na amani.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku hii yaliyoandaliwa katika kaunti ya Mombasa, mwenyekiti wa baraza la vyombo vya habari David Omwoyo amewahimiza waandishi wa habari, kutumia redio kueneza amani na kuwaunganisha wakenya.

Wakati huohuo vica jenerali wa jimbo katoliki la Eldoret padre William kosgey amewataka wanahabari kuzingatia maadili ya tasnia ya uanahabari wanapotekeleza majukumu yao.

Akizungumza na idhaa hii afisini mwake wakati alipoungana na wanahabari kusherekea siku ya redio kote ulimwenguni amesema kuwa wanahabari wanafaa kuweka misingi njema ya kufanya kazi yao katika kuwaelekeza wasikilizaji panapofaa.

Amewahimiza  wanahabari kutumia redio kama chombo cha amani  na kuwapa matumaini wasikilizaji huku akiwapa moyo wa kuepukana na changamoto ambazo zinawazingira kila wakati wakiwa kazini.

February 13, 2023