BY ISAYA BURUGU,5TH OCT,2023-Kenya imeungana na ulimwengu hivi leo kuadhimisha siku ya walimu duniani inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 5 Oktoba.Maadhimisho yam waka huu humu nchini yameandaliwa jijini Nairobi na kuongozwa na tume ya kuwajiri wlaimu nchini TSC.

Mkurugenzi mkuu wa tume hiyo Nancy Macharia amesema kuwa tume hiyo iko mbiyoni kuweka mikakati ya kuboresha utenda kazi wawalimu kote nchini.HUKU akiwashukuru walimu kwa juhudi zao zilizopelekea kalenda ya kimasomo kurejelewa nchini baada ya misukosuko iliyoletwa na janga la Corona,Bi Macharia amesema walimu watazidi kutambuliwa katika juhudi zao za kupiga jeki ustawi wa sekta ya elimu.

.Aidha ametangaza kuwa TSC hiyo kesho itaanza kuwapa mafunzo walimu wote walioajiriwa hivi maajuzi ili waweze kuwa katika nafasi nzuri kufundisha chini ya mtaala mpya wa CBC.

Kwa upande wake mwenyekiti wa tume ya TSC Jamleck Muturi amesema kuwa tume hiyo itaendelea kuunga mkono mageuzi katika sekta ya elimu nchini yanayoongozwa na serikali.

Muturi amepigia upatu mageuzi kwenye mifumo mbali mbali ikiwemo mtaala wa elimu akiongeza kuwa ni sharti kilakitu kiambatane na mageuzi yanayoshuhudiwa katika Nyanja ya elimu ulimwneguni. Kauli mbiyu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni walimu tuwatakao kwa elimu tunayoihitaji .

 

 

 

Share the love
October 5, 2023