BY ISAYA BURUGU,11TH MARCH,2023-Serikali ya kaunti ya Kajiado inapanga kupandisha hadhi baadhi ya vituo vyake vya Kafya katika kaunti hiyo ili kupiga jeki huduma za afya na kuwanufaisha wananchi. Akizungumza alipozuru hospitali ya rufaa ya Kajiado,

Waziri wa afya Alex Kilowa amesema tayari mchakato umeanza ambapo hospitali ya Mbirikanyi eneo la Loitoktok imepandishwa ngazi hadi kiwango cha level 4 na wanatarajia kupandisha ngazi hospitali zingine ili kuhakikisha kuwa huduma Zaidi zinapatikana karibu na wananchi.

Aidha ameongeza kuwa mpango wa kutatua changamoto za uhaba wa dawa katika hospitali mbali mbali unaendelea na kuwataka wananchi kutumia fursa hiyo na kunufaika na huduma mbali mbali zinazotolewa katika vituo mbali mbali vya kiafya Kajiado.

 

 

 

 

 

March 11, 2023