Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amepinga vikali hatua ya kuondolewa kwa marufuku ya utengenezaji na uingizaji wa vyakula vya kisaki au GMO.

Akiwahutubia waaandishi wa habari,Kalonzo amesema kuwa sayansi imedhihirisha vyakula hivyo si salama kwa afya ya binadamu.

Kalonzo ameongeza kuwa serikali ingepata maoni kutoka kwa wananchi na wakulima kabla ya kuondoa marufuku hiyo iliyowekwa miaka kumi iliyopita na hayati rais mstaafu Mwai Kibaki.

October 11, 2022